Mwongozo Wa Biashara Ya Mtandao Ya Kampuni Ya Green World Kwa Afrika Mashariki

Biashara Ya Mtandao

mkutano wa mwanza


Nini Maana Ya Biashara Ya Mtando

Kwa kifupi, biashara ya mtandao ni kazi ya kujenga mtandao (jumuia ya watu) wanaotumia bidhaa au huduma. Mtandao hujengwa kwa kuwashirikisha marafiki, ndugu au wanachama wengine watumie bidhaa au huduma hizo. Wanachama hao wakiwashirikisha wengine kutumia bidhaa au huduma hizo, mitandao ya biashara zao hukua na kuwa mikubwa zaidi na zaidi. Wanachama hulipwa kutokana na mauzo yao ya rejareja na kutokana na ukubwa wa bidhaa zinazouzwa rejareja na wanachama waliowafundisha na kuwaongoza katika mitandao yao.

Kwa takribani miaka 50 sasa, biashara ya mtandao imekuwa ikitoa fursa kwa watu waliotaka kuanza biashara zao ambazo wangeweza kuzifanya wakiwa majumbani kwao ili kujiongezea kipato na kuweza kumudu maisha yao. Ubunifu huu wa mfumo huu mpya wa kufanya biashara umekua na kufikia kuwa ni biashara yenye thamani ya dola bilioni 50 inayoshirikisha nyanja zote za uchumi kwenye nchi karibu zote zilizoendelea duniani.

Biashara Ya Mtandao Inafanyaje Kazi?

Watu waliofanikiwa kibiashara katika uwanja huu wametumia muda na nguvu zao kujifunza ili kujua ni nini kinahitajika ili kufanikiwa katika biashara hizi. Kama unataka kupata mafaniko kama waliyoyapata wao, ni busara kujifunza njia walizozigundua na kuzitumia. Jee, usingependa kujifunza kutoka kwao ili kujipunguzia muda wa kufanya utafiti wako wewe mwenyewe? Wafanya biashara wa mfumo wa kizamani (traditional business ) hawangeweza kupoteza muda wao na nguvu zao kwa ajili yako kwa sababu hawana la kunufaika kutoka kwako.

Hii ndiyo tofauti ya biashara ya mtandao. Wafanya biashara waliofanikiwa kwenye biashara za mtandao wanapata faida pale wanapowafundisha watu wengine waliojiunga na biashara hii mbinu za kufikia mafanikio kama walivyofanya wao. Hii inaitwa Nadharia Ya Mwendelezo (Priciple Of Duplication), na maana yake ni kuwafundisha watu wengine kile ulichokifanya wewe ili kuendeleza mafanikio yako. Ndani ya Green World kuna faida nyingi mno za kufanya hivyo.

Kwanza, unaanza kupata mafanikio kwa kujiunga na kuwa mwanachama wa Green World. Kisha unawafundisha watu wa timu yako - watu mahiri waliojiunga chini yako (uzao wako wa kwanza) kwa nia ya kubadili maisha yao - kufuata hatua rahisi ulizotumia na kuendeleza mafanikio yako. Halafu, ukiwa karibu yao, kila mmoja wao atawafundisha wafuasi wake ambao nao watawafundisha walio chini yao. Punde si punde, unakuwa umejijengea jumuia ya wafanyabiashara na kufikia mafanikio ya kiuchumi kama yanavyotolewa na kampuni ya Green World.

ofisi za green world

Kwa Nini Green World Ilichagua Biashara Ya Mtandao?

Mfumo wa biashara ya mtandao unatoa faida nyingi kwa watengenezaji wa bidhaa, wagavi na wafanya biashara:

Kuwasilisha Bidhaa. Mfumo wa biashara ya mtandao unafanya kazi kubwa sana ya kuwasilisha bidhaa kwa wateja (walaji) .... kwa sababu unaorodhesha kikosi kikubwa cha watu hodari kwenye kampuni ambao wanaanza kunufaika mara moja na kupata mafao kulingana na muda wao waliouwekeza kwenye biashara, na ujuzi ambao wameupata. Mtindo wa biashara ya mtandao wa mtu kwa mtu una uwezo wa kuwaelimisha walaji kwa kiwango ambacho matangazo ya biashara hayawezi kukifikia. Unawawezesha walaji kujua undani wa bidhaa zinazouzwa - ni aina ya biashara yenye mafanikio makubwa.

Bei nafuu. Biashara ya mtandao imependwa na wenye viwanda na wafanya biashara kutokana na kuondokewa na gharama kubwa za kuweka matangazo makubwa na utunzaji wa bidhaa .... na kwa wanachama wa kampuni hizo, wamenufaika kutokana na kulipwa pesa ambayo ingetumika kwa ajili ya matangazo ya TV na usafirishaji wa vifurushi.

Ushirikishwaji Kibiashara. Maendeleo ya teknolojia za kompyuta na mawasiliano yamewezesha wanachama kufuatilia malipo yao, kuweka vizuri biashara zao na kufanya mawasiliano na wanachama wa juu na wa chini katika mitandao yao.

Kwa kifupi, lilikuwa ni wazo zuri sana la kibiashara.

Faida Za Biashara Ya Mtandao Kwako

Jambo la msingi zaidi kuliko lile la namna biashara ya mtandao inavyobadilisha namna ya utangazaji na uuzaji, ni jinsi gani biashara hiyo itakupa faida wewe!


Biashara Ya Mtandao Ya Green World Inakufanya Kuwa Mwamuzi Wa Biashara Yako


Katika kampuni ya Green World unahodhi faida zote zinazotolewa na biashara ya mtandao ya asili ..... na unapata faida zote za mpango mpya wa malipo wa Green World na bidhaa/huduma! Kama ilivyo kwa biashara nyingine yo yote ya mtandao, unakuwa mwenye maamuzi yote baada ya kujenga jumuia yako ya wafanya biashara. Unakuwa mkurugenzi wa biashara yako. Unatoa maamuzi yote. Unaamua ni lini, wapi na kwa kiasi gani unataka kufanya kazi. Unajipangia malengo yako ya biashara na ni vipi unataka kuyafikia. Kwa maneno mengine wewe ndiyo kila kitu! Kwa vile kampuni ya Green World itakupa zana zote za kibiashara na mpango wa biashara wa kukuwezesha kupata mafanikio, kinachohitajika kwako wewe ni dhamira ya kufanya kazi kuyafikia malengo yako ndani ya Green World.

Images/green world office dsmBiashara Ya Mtandao Ya Green World Inakupa Fursa Adimu Ya Kipesa

Nadharia ya biashara ya mtandao inatoa uwezo wa kuchagua fursa tofauti za kifedha ..... na fursa ya kampuni ya Green World inakidhi haja hiyo. Unaweza kupata faida kubwa ya rejareja kwa kuuza bidhaa na huduma za kampuni hii kwa rejareja kwa watu unaokutana nao au kuwajua. Au, unaweza kujipatia kiasi kikubwa zaidi cha pesa kwa kuwashawishi wateja wako kujiunga na jumuia ya wafanya biashara ya kampuni ya Green World.


Biashara Ya Mtandao Ya Green World Ni Namna Ya Kufanya Biashara Binafsi.


Wengi wa watu utakaokutana nao katika mtandao wako wa biashara ya Green World watakuwa ni wanafamilia, ndugu na wanachama wenzako - watu uwapendao na unaopenda kufanya nao kazi! Utakapowaona watu hawa wanaona shauku uliyo nayo jinsi unavyopata mafanikio, furaha na kujiamini kwako kutaongezeka.


Biashara Ya mtandao Ya Green World Ni Biashara Ya Kizazi Kipya


Biashara ya mtandao ni moja fursa za biashara zinazotoa faida kubwa na zinazokua kwa haraka sana duniani kwa sasa. Kuanzia sasa na siku za baadaye, mitambo ya utoaji habari ya teknolojia ya hali ya juu iliyoundwa mahsusi kwa biashara za mitandao, itawezesha ufanisi wa biashara ya bidhaa na huduma katika kumfikia mteja au mlaji.





<<<< MWANZO